readenglishbook.com » Religion » Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗

Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗». Author Susan Davis



1 ... 3 4 5 6 7 8 9 10 11 ... 17
Go to page:
tu kwake. Mimi sio mtu anayamkujia tu mara moja moja au wakati anahitaji kitu kutoka kwangu. Tumeshikamana. Nikisonga, anasonga. Tunachanganyika. Tu kitu kimoja. Yu kwenye mapenzi yangu na anatembea kwenye njia yangu nyembamba. Mwendo wake na wangu unawiana.

Kwa hivyo wanangu, nawaachia uchaguzi. Ingawa ningependa mnichague, mngali mna hiari. Kwa hivyo ninawaalika mje kwenye uhusiano mkamilifu na kusudi nililowaumbia. Uchaguzi ni wenu. Msingojee sana kuchagua. Toleo hili ni la muda mfupi, halitakuweko milele.

 

SURA YA 10: TAMAA YA ULIMWENGU

Ndiyo binti. Natuanze. Susan, hili ndilo jambo ninalotaka kuzungumzia leo: Dhambi itokayo mioyoni mwa wanadamu – na dhambi ya tamaa ya ulimwengu. Njia zote za dunia ni mbovu, waja waovu wanaoendeleza vitendo vya uovu. Yote dunia itendayo ni mbali na Mungu. Dunia haiko kwenye mapenzi yangu. Dunia hukiri kunijua, bali i mbali sana nami, na ukweli wangu. Inakimbia kwa kasi kuelekea inakotaka kwenda bila ushauri wangu, niliyeiumba. Huu ni uovu. Kukimbilia nje ya mapenzi yangu ni uovu. Mapenzi yangu tu ndiyo mema. Hamuyaoni haya wanangu? Dunia hii itawezaje kuelekea kwa Mungu ikiwa imeniacha mimi Mungu na mambo yote ninayosimamia? Nasimamia utakatifu, usafi wa moyo, sheria na taratibu, ukweli na uadilifu. Dunia hii inapinga njia zangu na hata haikaribiani na yale kitabu changu kinaweka kama ukweli na njia zangu za milele. Dunia inanikashifu na kuzikashifu njia zangu ipatapo njia ya kufanya hivyo. Inawakashifu wanifuatao. Njia zangu haziheshimiwi wala kutukuzwa. Zingalikuwa zinaheshimiwa, dunia haingalikumbwa na huzuni, mateso, magonjwa na masikitiko. Njia zangu zaleta baraka. Njia za ulimwengu zinaleta laana tele. Ni wale tu ambao wanatembea karibu nami na neno langu ndio wapatao amani na utulivu niwapao hata wakiwa taabani.

Huyu ndiye bi arusi wangu anifuataye bila kusita. Anijua. Anipenda. Haendi mbali nami. Anajua ya kwamba mimi ndiye chanzo cha maisha yake, nguvu zake, upendo wake, na uwezo wake. Ni wapi kwingine atakakokwenda ili apate faraja kama hii? Anajua ni vyema kukaa nami kuliko kuwaendea wapenzi wengine. Amenijaribu, akanionja na anajua mimi ni mwaminifu kwake. Ni wake kwa jumla. Hakuna awezaye kupachukua pahala pangu machoni mwake. Dunia haijui upendo wangu. Imekubali mapenzi duni. Ole wao wafuatao dunia na njia zake wakiamini kuwa mfumo wa dunia una majibu yote! Hivi karibuni, dunia itaipoteza nuru yake ya mwisho nitakapomuondoa bi arusi kati yao. Atakapo ondoka, dunia itabaki gizani. Hakutakuwa na chochote cha kutazamia kinachoweza kuwaelekeza kwa ukweli na uzuri. Ubaya na uovu ndio utakuwa duniani. Hii ndiyo dunia itakayokuja hivi karibuni. Haya yatafanyika hivi karibuni.

2 Wathesalonike 3:3-4. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kitu kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

2 Wathesalonike 2:6-7. Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

Dunia ambayo haishi kwa kufuata sheria na maadili yangu ni kama meli bila usukani. Hii ni meli ambayo imekufa, meli ambayo inazama. Wanangu, hivi karibuni, mtaona kifo na maangamizi ambayo hamjawahi kuona maishani mwenu. Maanake dunia hii imechagua kumgeuka Mungu wake. Muumba wake. Msipumbazwe. Ulimwengu hauwezi kuendelea bila maadili na ukweli wangu. Ni meli inayozama. Ni wakati wa kuondoka kwenye meli hii inayozama. Mtakuja nitakapowaita waumini wangu? Mtanifuata ama mtabaki nyuma mkikwamilia kwa matumaini yasiyo ya kweli kuwa dunia ina majibu yote? Mngali mnawasikiza mbwa mwitu waliovalia ngozi ya kondoo wanaowahadaa na kuwambia kuwa kila kitu ki sawa? Hawa mbwa mwitu wasionijua, wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake. Mtaendelea kupotoshwa na kupofuka kwa sababu mnaufurahia ulimwengu sana?

2 Timotheo 3:5. Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake.

Njooni mshiriki na Mungu na mgundue kuwa kuna ukweli mkuu, kuna amani kuu, kuna upendo mkuu. Ni miye! Nifuateni wana! Nijueni. Ninastahili kufuatwa. Ninastahili kujulikana. Nipeni muda wenu. Mimi ndiye niliyewaumba. Hamtaki kukaa nami milele? Kuna njia nyingine. Ni mahali ambapo wema wote utokao kwangu unakosekana. Ndiyo. Yote yaliyo mema duniani hutoka kwangu.

Niliumba vyote. Bila mimi, hamtapata tena wema huo wote, vitu vyote vilivyo vizuri mnavyovifurahia vitokavyo moyoni mwa Mungu. Kwa hivyo, yatafakari haya sana. Amueni: milele nami au bila mimi. Amueni. Chagueni. Je, nitawachukua nitakapokuja kumchukua bi arusi wangu? Ni uamuzi wenu. Bali kuna malipo. Ni sharti muachane na ulimwengu na anasa zote za ulimwengu kwa maana njia za ulimwengu sio njia zangu. Nitawaachia ninyi wenyewe muamue mtakako kwenda. Ni wachache sana wanaochagua njia yangu. Wachache sana ...

1 Yohana 2:15. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

 

 

SURA YA 11: DUNIA INAELEKEA KWENYE DHIKI

Natuanze binti yangu. Sasa nataka kuzungumzia juu ya mambo ambayo yatatendeka hivi karibuni. Dunia inaelekea kwa matatizo. Kuna mawingu makuu meusi kila upande. Karibuni, hivi karibuni, dunia hii itabadilika. Yote yatabadilika kwa ghafla bi arusi atakapoondolewa. Dunia itakuwa na giza na bila matumaini ya kurudia ilivyokuwa hapo awali. Hivi karibuni, wanangu, jambo hili litatendeka. Anzeni kujitayarisha. Mimi sio wa kutia chumvi kwa ukweli. Maneno yangu niyakuaminika. Wakati wa mabadiliko haya waja upesi sana. Mwendo umeshapangwa na hauwezi kubadilishwa. Dunia imekuwa mbovu na hakuna mtu, serikali, wala nguvu zo zote zile zitaweza kusimamisha yajayo. Huu ni wakati wa ufunuo na siku za mwisho. Wakati wa kurudi kwa mwanangu. Hivi karibuni, dunia itajua yaliyotendeka kama mwizi usiku. Hakuna lolote linaloweza kupinga tukio hili. Ilishatabiriwa na sasa yaja kutimia, jinsi maneno yangu yalivyosema kuwa itatendeka.

1 Wathesalonike 5:2. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.

Wana, mnahitaji kufanya matayarisho. Jitayarisheni. Jitayarisheni kwa kurudi kwangu hivi karibuni, na kurudi kwa mwanangu. Yuaja na jeshi la malaika wake mawinguni ili kumtwaa mpendwa wake. Wakati huu umekaribia. Amkeni enyi waumini. Jitayarisheni. Jitayarisheni kwa tukio kuu kwenye historia, Bwana arusi akimjia bi arusi. Njooni mjitayarishe. Nyote mjitayarishe. Njooni mtayarishwe na damu ya Mwana Kondoo. Jifunikeni kwa damu yake. Damu inapatikana bure. Jitoleeni katika upendo wake mkuu. Mfanyeni mwanzo na mwisho wenu. Tu kitu kimoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa wanangu, adui ana mipango yake. Anajitayarisha kuzindua mashambulizi yake dhidi ya wanadamu. Ustaarabu wote u karibu kubadilika. Sitaki mpatwe kwa kutokujua. Bali mageuzi haya makubwa yatatendeka hivi karibuni. Mnahitaji kujitayarisha. Binadamu watashuka wawe na kichaa na maovu yasiyoweza kutibiwa. Hadi mwanangu atakaporudi duniani ndipo maovu yatamalizika.

2 Wathesalonike 2:8. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake.

Hivi karibuni wanangu, mtahitajika kufikia mapatano: Mtaamini nini? Mtashikilia nini? Ulimwengu ambao unaisha au njia zangu na mapenzi yangu? Nawapa ufalme wa milele. Msidhani ulimwengu una mema ya kuwapa. Ulimwengu u karibu kwisha. Mandhari yake yatabadilika. Msiwe na tamaa mkishikilia ulimwengu usio na mategemeo. Mnapoteza wakati wenu. Ukubali ukweli huu na mwamke. Nawapa ukweli. Someni kitabu changu mkilinganisha na yatendekayo sasa hivi. Ni sawia kabisa maanake yaliyotabiriwa kale lazima yatimizwe. Sio ulinganifu wa kibahati. Hili ni lile neno kuu la Mungu ambalo linatimia. Neno langu halikosi kutimizika. Maneno yangu ni stadi. Mimi ni Mungu mwenye nguvu zote, mwenye ukweli, nisiyepunguza hasira, mwenye uwezo wote, mfalme wa wafalme asiyebadilika, Bwana wa mabwana. Maneno yangu hayabadiliki.

1 Petero 1:24-25. Maana, mwili wote ni kama majani, na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka. Bali neno la Mungu hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Aliyelala naamke! Huu ndio wakati wa kuamka. Muwe macho. Wakati ni sasa. Ondoeni vyote vinvyowapofusha. Wekeni chini mambo ya dunia na kunisikiza kwa makini. Saa sita ya usiku yakaribia. Wanangu, nawasihi, msipatikane mkiwa hamjajitayarisha. Jitayarisheni. Wakati wa Mwana kurudi u karibu ....

 

SURA YA 12: KURUDI KWANGU HIVI KARIBUNI

Natuanze. Binti yangu, leo ninataka kuzungumzia juu ya yale yanayohusu dunia kwa ajili ya kurudi kwangu hivi karibuni. Dunia i karibu kushuhudia mlipuko wa mabadiliko. Mabadiliko yaja kutoka pande zote. Kuondolewa kwa bi arusi wangu – wale ambao wamejitayarisha. Wamejitakasa na damu yangu pia kupitia kuoshwa na neno langu. Kutolewa kwa bi arusi kutafuatiwa na uteketezi wa ghafla na kupanda kwa mfumo wa mpinga Kristo.

Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Haya yatakuwa mabadiliko ya ghafla. Hakuna cho chote kitakachokuwa kikuu kuliko mabadiliko haya katika historia. Watakaoachwa watahisi mabadiliko haya na watakaochukuliwa watajua. Wengi watafariki katika mabadiliko haya maana uharibifu waja ulimwenguni. Uharibifu hautakoma kwa maana nitamwaga ghadhabu yangu duniani. Yale ambayo yanafanyika sasa hivi ni kionjo tu cha yale yajayo. Ndio maana ninaendelea kuwaonya kupitia ishara mzionazo na pia kupitia kwa watumishi wangu: vijana kwa wazee wote pamoja. Maonyo yangu yamekuwa wazi na thabiti, kupitia kwa neno langu na maonyo ninayotoa kupitia kwa wengine. Sibadiliki. Mimi ni ukweli udumuo milele. Ukweli wangu haubadiliki. Neno langu halibadiliki.

Wanangu, wakati umetimia. Ni wakati sasa wa kuwaonya wale walio karibu nanyi. Msinyamaze. Waelezeni kuhusu maangamizi yajayo duniani. Wengi wanadhani kitabu change ni hekaya, au hadithi kuu, bali kila neno lililomo ni kweli na litatendeka. Hivi karibuni, kitabu cha ufunuo kitaanza kutendeka kama kilivyopangwa. Mtayaona yote yakitukia machoni penu. Tayari yameanza kutendeka ikiwa mtachukua wakati wenu kukisoma na kuangalia dunia inavyoenda. 

Yote yanayotendeka yalitabiriwa kitambo sana. Yawekeni mashaka yenu kando. Acheni kuwasikiza wasionijua. Kila mmoja wenu ajisomee kitabu change. Mtafuteni Roho wangu Mtakatifu kuwaangazia ukweli, kuwapa marhamu ya macho—haya ndiyo mnayohitaji ili muone ukweli.

Ufunuo 3:18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

Sitaki mpatwe ghafla. Nawataka muwe macho muujue ukweli ili muwe tayari. Nawataka wanangu waje kwa nuru a kuona ukweli upo. Upo. Hamna sababu ya kubaki kwenye giza bila kuwa tayari kwa yale yajayo. Naweza kuwaongoza. Niacheni niwaongoze. Natamani kuwaongoza. Natamani kuwashika na kuwaonyesha kuwa mnaweza kuhepa maafa yajayo duniani. Yote hayajapotea.

1 ... 3 4 5 6 7 8 9 10 11 ... 17
Go to page:

Free e-book «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗» - read online now

Comments (0)

There are no comments yet. You can be the first!
Add a comment