Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗». Author Susan Davis
Natuanze. Haya maneno ni kwa yeyote yule atakaye yapokea. Leo nitazungumzia kuhusu unyakuo ujao na kuondoka kwa bi arusi wangu, Kanisa langu.
Huu wakati unakaribia kwa upesi. Wanangu wengi hawako tayari. Wananipinga na kukwamilia kwa dunia. Wanataka kutembea kwenye njia za dunia. Wanakimbia hapa na pale na hawasikii maonyo niwapayo. Hivi karibuni nitaacha kuwaonya kisha nije na bi arusi ataondolewa. Atatolewa kabisa hapa duniani.
Danieli 12:4. Lakini wewe, ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.
Hatambuliki duniani. Amefichwa. Nimemweka utawani kwa usalama. Nuru yangu inaangaza kupitia kwake – Nuru ya mwisho ambayo imebaki duniani. Muda ni mfupi na hivi karibuni nuru hii itazimika. Watumwa wangu wataondoka kwenda kwa makao yao ya usalama mbinguni wauache huu ulimwengu wa udhalimu.
Unyakuo huu utakuwa tukio kubwa. Kuondolewa kwa wanangu walio tayari. Hakutakuwa na tukio lingine kubwa kama hili kwenye historia ya binadanu. Hakutakuwa na jambo jingine kama hili, kabla na badaye. Huku ndiko “Kutoka” kukuu.
Wanangu wataondoka mara moja na kupokea miili mitukufu. Miili hii itakuwa thabiti na ya milele. Itakuwa kama mwili wangu mtukufu. Mimi ndiye limbuko kwa wengine wengi. Hawa wana watakuwa na maisha ambayo hawajawahi kuwa nayo mbeleni. Maisha matukufu, uzima wa milele.
1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tatabadilika kwa dakika moja. Kufumbua na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwa kushindwa.
Kutakuwa na vitu vingi vyema sana mbele kwa wanangu watakaonyakuliwa. Acheni niwaonyeshe kidogo tu vile itavyokuwa: Wanangu watakapofika, watalakiwa na wapendwa wao: familia na marafiki wale tayari wako mbinguni. Nitakuwa nikiwatazama. Huu utakuwa wakati wa utukufu mkuu. Ni tunu ilioje kuungana na familia ulioikosa muda mrefu! Kisha wanangu watapelekwa hadi kwenye karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Nitawaongoza kwenye karamu hii.
Ufunuo wa Yohana 19:9. Naye akaniambia, Andika Heri walioalikwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Meza itaandaliwa kwa vitu tele. Vikorokoro vyote vitakuwako. Kila jambo kuhusu karamu hii litakuwa la kuwastaajabisha. Wanangu watakaa katika sehemu iliyoandaliwa kila mmoja wao na majina yao yatakuwa yameandikwa kwenye sehemu hiyo kwa dhahabu. Vyombo vyote vitakuwa vya dhahabu vilivyopambwa na vito. Kitambaa cha mezani kutakuwa cha hariri, na nyuzi za dhahabu. Nuru itang’aa na vikombe vyote vitakuwa vya dhahabu vilivyolainishwa na vito ukingoni.
Kutakuwa na zawadi kwa kila mmoja pahali watakapoketi. Zawadi hii itakuwa ni kumbusho la uhusiano wangu na huyo mwanangu. Kila zawadi itatofautiana na nyingine. Kila zawadi itakuwa na maana yake kwa kila mwana kuonyesa uhusiano wangu naye. Kutakuwa na vitu vingi vya kustaajabisha siku hiyo – siku ya karamu ya arusi yangu.
Mathayo Mtakatifu 22:2. Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.
Kila mwana atakuwa na malaika wa kumshughulikia. Chakula kinatengenezwa kwenye jikoni zangu za mbinguni. Hakuna kitakachokosekana. Vyakula vyote vitakuwa vya kipimo cha mbinguni. Kutakuwa na vyakula muvijuavyo kutoka kwenye ardhi na pia vya mbinguni ambavyo hamjawahi kuviona. Kutakuwa na uzuri usio kifani.
Meza yangu itajaa mwangaza: Mishuma na Menorah (kinara cha taa saba). Wanangu watavaa kanzu za mianga. Watatoa mianga na hakutakuwa na vivuli.
Waraka wa Yakobo 1:17. Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Bwana wa mianga; kwake hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeukageuka.
Nitaongoza kwa kumpongeza bi arusi wangu. Nitaimba sifa zake kwa maana yeye ni mrembo kwangu. Kutakuwa na muziki na dansi na furaha kila mahali.
Bi arusi ataniona kwenye utukufu wangu wote. Kwa maana nitakuwa ninang’ara ajabu. Uzuri wangu utang’aa kila mahali na upendo wangu utatiririka kwa wote ambao watashiriki kwenye karamu hii. Babangu atakuwa akitutazama kwa furaha na raha kuu kwa maana kutakuwa na kucheza na furaha tele.
Nitacheza dansi na bi arusi wangu na tutakuwa kama kitu kimoja. Wanangu watacheza na kufurahia. Mioyo yote itakuwa yenye furaha. Hakuna atakayekuwa na huzuni. Huu utakuwa wakati mukuu wa utukufu na upendo.
Njiwa watajaa hewani. Watapaa kwenye mapambo na kuumba mipangilio iliyo na ujumbe kwa bi arusi wangu hewani. Bi arusi atashikwa na bumbwazi. Nitampa bi arusi wangu pete. Majina yetu yatakuwa yameandikwa kwenye pete hizi. Maua ya kila aina na rangi yatakuwa kila pahali. Rangi mpya na rangi nzee. Harufu nzuri itajaa hewani. Wanangu watafurahia mno.
Luka 15:22. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, lileteni upesi vazi lililo bora mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni.
Malaika wangu watajaza mbinguni na nyimbo, kucheza na muziki. Vifaa vya muziki vya mbinguni vitacheza muziki mzuri. Hata nyota zitaimba zikisherekea Mwana Kondoo na bi arusi wake.
Ayubu 38:6-7. Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
Majeshi yote ya mbinguni yatakusanyika na kuimba sifa kwa bi arusi wa Mwana-Kondoo. Kila mmoja ataimba sifa kwa Mfalme, bi arusi wake yuaja. Amejiweka tayari. Furaha na ianze!
Ufunuo wa Yohana 19:7. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja na mkewe amejiweka tayari. Mwana Kondoo aichukuaye dhambi ya dunia ameungana na mpendwa wake kwa ndoa takatifu. Jina lake ni kuu! Lisifuni jina lake takatifu kati ya mbinguni zote kwa maana amemchumbia mpendwa wake naye amempa moyo wake!
Yohana 1:29. Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Wanangu pia wataonyeshwa makao yao. O! binti, ni uzuri, ni fahari. Hakuna jicho ambalo limeona wala sikio ambalo limesikia aliyoandaliwa bi arusi wangu mtukufu anipendaye.
1 Wakorintho 2:9. Lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
Binti, makao haya yatakuwa yakupendeza sana kuliko chochote kile ulimwengu unaweza kuwapa. Hakuna cha kulinganisha na yote yale nimemwandalia bi arusi wangu. Makao hayo yatamfaa kila mwana. Hakuna makao yatakayofanana. Kila nyumba itakuwa tofauti na nyingine.
Yohana Mtakatifu 14:2-3. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia, maana naendea kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Wanangu wataduwazwa na kile watakachokipata kwa kila nyumba. Kila nyumba ina vitu vitakavyompendeza na kumfurahisha mwenyewe. Hakuna kitu ardhini kinachoweza kueleza mapambo na uzuri wa kila moja ya nyumba hizi. Tutashiriki pamoja. Tutacheka na kutalii pamoja. Msisimuko hautakwisha.
Kutakuwa na bustani na starehe kokote. Muziki utajaa hewani na harufu nzuri. Kila nyumba itajaa vicheko na mapenzi. Hakutakuwa na ukiwa mbinguni. Ni pamoja na wanangu kila mara tukifurahia na kukaa pamoja.
Zaburi 36:8. Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako, Nawe utawanywesha mto wa furaha zako.
Upendo wangu utawazunguka kote. Kicheko, upendo na furaha ndio tuzo ya hizi nyumba za kudumu milele. Furaha isiyo kifani, raha idumuyo milele.
Hiki ni kionjo tu cha yale yajayo. Wanangu hawana ufahamu kuhusu yale niliyowaandalia. Hakuna vile niwezavyo kuwaelezea yaliyo juu mbiguni kikamilifu. Kuweko na kushuhudia pekee ndiko kutaweza kuwapa picha kamili.
Kwa hivyo wanangu, njooni mfurahie uzuri wa mbinguni kwenye ufalme udumuo milele na nyumba zilizotenganezwa kwa upendo za bi arusi wangu.
Zaburi 16:11. Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume, mna mema ya milele.
SURA YA 8: JITAYARISHENI KWA UNYAKUO
Natuanze. Sasa binti, siku zijazo kabla ya unyakuo, kuna mengi yakutayarisha. Wanangu wanafaa wawe na muda nami katika mahali pa siri. Muda wa utulivu, ili waweze kunijua. Nawahitaji kwa pamoja nami. Ningependa kuwaelezea yaliyo moyoni mwangu. Nataka wanipe mioyo yao kikamilifu, maisha yao na vyote vile wamevishikilia hapa duniani.
Zaburi 91:1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu, atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Wanangu wameushikilia ulimwengu. Wanaamini kuwa ulimwengu utawapa kila kitu. Ulimwengu ni mtupu na wenye moyo baridi. Kila mtu kibinafsi. Hakuna amjaliye mwenziwe. Imekuwa hali ya unyang’au. Kila mmjoa anamfuata mwenziwe kusudi apate kile anachotaka kwake na kujitosheleza binafsi. Ni ulimwengu usio na matumaini na wa taabu nyingi. Na wanangu wangali wanaushikilia wakiamini utawapa watakayo. Wanapumbazwa na waliopotea ambao wanaeneza njia zao potovu. Wanangu wanafaa wajiondoe kwenye upuuzi huu na wanirudie mimi Mungu Aishiye, Muumba wao, aliye na majibu yote ya maisha ya sasa na yajayo.
Mimi ndiye Mungu Mkuu wa vyote viishivyo na roho zote zinazopumua. Nina funguo za uzima wa milele. Jisalimisheni, kwangu nijapo kuja duniani, nimchukue bi arusi wangu na kuwaondokea ili ulimwengu upokee hukumu yake.
Ayubu 12:10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote.
Haya yote yatatendeka hivi karibuni. Kusalimu amri ndiko kunakohitajika ili muwe kati ya bi arusi wangu; wanangu nitakaowaokoa. Hakuna lingine. Mnitii kwa kila jambo na mwache nitawale kila sehemu ya maisha yenu ndipo roho wangu atakuja kwa roho zenu na kuwafanya upya na kuisafisha mioyo yenu kwa kuifunika kwa damu yangu iliyotoa fidia na uongofu kupitia kwa neno langu. Hii ni muhimu ili kuzikomboa nafsi zenu ili ziwe bila doa, ziwe safi na tayari kwa unyakuo, kupelekwa mahali salama. Ikiwa mna mashaka au tashwishi yoyote, lisomeni neno langu!
Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akijitoa kwa ajili yake; ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Ombeni ili mjazwe na Roho Mtakatifu. Tubuni dhambi zenu. Anzeni kufunga ili kuonyesha majuto kwa dhambi zenu ambazo mumezileta mbele yangu, mimi Mungu aliye Mtakatifu. Nitawajaza tena. Nitawaongoza kwa ukweli wa milele katika njia zangu na mapenzi yangu.
Hiari zenu wenyewe zitawapeleka kwenye upotovu. Hii ndiyo njia pana ambayo neno langu linazungumzia. Njooni kwenye mapenzi yangu. Hii ndiyo njia nyembamba, njia iliyo salama na nitawapeleka kwa hiyo njia.
Mathayo Mtakatifu 7:13-14. Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, nayo njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Neno langu litawaongoza kwa njia yenye nuru. Njia zingine zote zinaelekea kwenye upotovu wa milele. Njooni kwenye nuru yangu na kwa mapenzi yangu. Nipeni uzima wenu. Niacheni niziondoe dhambi zenu mlizotenda na niwaonyeshe njia itakayowaongoza kwa uhuru ikiwatoa kwa utumwa wa dhambi.
Zaburi 119:105. Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Hata liweje, dhambi hukuweka utumwani, na kukufanya mtumwa wa dhambi. Naweza kuwaweka huru, bali ni lazima mjisalimishe kwangu, mtubu, na kukubali kuwa ninyi ni wenye dhambi na mnataka kuwekwa huru na mfanye hivyo kwa moyo uliojuta na ulio mnyofu. Nitafurahia kuwaweka huru kutoka kwa dhambi ambazo zinawafunga na kuwafanya watumwa. Mimi ninaweza kuwaweka huru kutoka kwa cho chote kile kinacho wafanya kuwa wafungwa.
Hamna jambo nisiloliweza. Hamna! Nilikuja kwa ajili ya wafungwa waliofungwa! Mnachohitaji kufanya ni kuniuliza tu, nami nitawaweka huru!
Luka Mtakatifu 1:37. Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.
Niacheni niwaondolee mzigo huu. Niacheni niwaondolee huzuni na simanzi. Niacheni niwaliwaze na kuichukwa mizigo yenu. Niacheni niwatayarishe kwa kurudi kwangu kutukufu! Yote haya ni yenu -- jitoleeni, wekani kando matamanio yenu yote ya kilimwengu na mje kwangu kwa kujitolea kikamilifu. Nitawapa amani ipitayo akili zote na mtakuwa sawa mbele zangu. Mtakuwa bila hukumu mbele yangu, mbele ya Baba na mbele ya Roho Mtakatifu.
Wafilipi 4:7. Na amani ya Mungu,ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
Upendo huu hawezi kununuliwa --- ni wa bure --- bure kwenu kuupokea – bure kwenu mkiuliza. Harakisheni kwa maana ni wa muda mfupi. Nakaribia kurudi,
Comments (0)