Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗». Author Susan Davis
Imani kama ya mtoto ndiyo yenye maana, kwa sababu mtoto hakimbii mbele. Mtoto humfuata mzazi nyuma na kwa karibu kwa sababu ana imani na mzazi wake. Anamkwamilia mzazi akimngoja amuongoze na kumfunza. Mtoto haichukui nafasi ya mzazi. Anafahamu vyema kuwa hawezi kuongoza. Ana imani kuwa mzazi wake atakutana na mahitaji yake yote. Mtoto anapoenda mbali na mzazi wake, anakuwa na wasiwasi na mahangiko maanake anafahamu kuwa yule mzazi wake ambaye anamwamini na kumpenda ndiye tu anayeweza kukutana mahitaji yake yote. Hivi ndivyo uhusiano ulivyo kati ya Mungu na yule mtumishi wake myenyekevu. Watu wanyenyekevu humfuata Mungu kama vipofu maanake wamwamini, naye Mungu huwakomboa.
Hamna majibu kwingine. Mungu ndiye Mkuu na ndiye Tumaini la pekee. Tumaini la kutegemewa. Watoto huwatafuata wazazi ili wawatimizie mahitaji yao yote. Wanawalilia maanake wazazi wao watawakomboa kama vile Mungu awakomboao wanyenyekevu wake wamfuatao kwa moyo mnyenyekevu na safi.
Je, unayaelewa haya binti yangu? Je, mtu aliye na kiburi anaweza kubadilika na kuwa mnyenyekevu? Binti yangu jibu ni “ndiyo” kwa kuongozwa na kunitii mimi, Mungu wenu.
Kwa hivyo, yote yanawezekana kwa Mungu. Ndiyo, yote yawezekana kwangu.
Mithali 15:33. Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima. Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Haya tuanza. Unyenyekevu ni upendo. Upendo unatokana kwa moyo mnyenyekevu. Upendo hautoki kwa kiburi. Kiburi huharibu upendo. Kiburi husema:
“Mimi ni bora kukuliko”.
“Najua mengi kukuliko”
“Haustahili mengi kuniliko”
“Hauna thamani kuniliko”
“Mimi naweza kujisimamia na “sikuhitaji”.
Kiburi kinasimamia haya yote, mwanangu.
Kiburi ni kibaya kwa njia zote. Ni kujifikiria mwenyewe tu, ni kujipendekeza, ubinafsi na mizizi yake iko kwenye uovu. Utukufu usio na maana unajipandisha juu ya Mungu na kujidai “Simuhitaji Mungu” Mimi ni Mungu. Najitawala. Kiburi huchukiza mno. Hamna uzuri wowote kwenye kiburi. Hakuna wokuvu kwa kiburi. Kiburi kina wazuia wengine. Kinawafanya wengine wajione duni wasiopendwa, wanakataliwa, wanaumizwa na kukwazwa. Kiburi ni tofauti sana na tabia za Kristo. Hakuna ukristo wowote katika kiburi. Hakuna kitu cho chote kizuri kitokacho kwenye kiburi – ni uovu mtupu. Unanielewa mwanangu? Je, twawezaje kutoroka kiburi Bwana? Binti yangu, kimbia mbali na kiburi, toroka kabisa uende mbali na kiburi. Tafuta unyenyekevu wakati wote.
Binti yangu, hauna haja ya kujipendekeza kwa watu ikiwa una mapenzi yangu.
Tafuta pendo langu na utosheke nalo na tamaa yo yote ile ya kutaka mapenzi kutoka kwa walio kuzunguka itafunikwa na hili pendo langu kuu. Waliokuzunguka, hawawezi kutosheleza mahitaji yako ya ndani. Mimi tu pekee. Mimi ndiye niwezaye kutosheleza moyo ulio na njaa, tupu na unao tamania.
Nina majibu yote ya moyo kama huu. Mimi ndiye pekee naweza kuujaza. wanadamu hawawezi. Hawana huo uwezo ingawa huwa wanaonekana kama kwamba wanao. Kukubaliwa na watu ni kwa muda mfupi tu. Mimi ndicho kisima kijazacho kote. Najaza na kutosheleka hamu ya moyo wa binadamu. Njooni kwangu ili mtosheleze haja zenu za mapenzi. Wekeni kiburi chini. Ni nguvu zinazoharibu upendo. Zinatenda nje ya upendo na kuharibu kila mtu. Kiburi ndio uovu wa kwanza. Bado kinatawala na kuishi katika mioyo ya binadamu. Kiburi kinawafanya wanadamu watafute njia zilizo tofauti na mapenzi ya Mungu.
Binadamu hujijenga kwa kutumia ngazi zao kazini, mali, talanta, walivyonavyo, na uhusiano na wengine. Hii ni miungu na inawafanya wasimtazamie Bwana Mungu kwa majibu kuhusu maisha yao. Wajijenga wa kutumia njia ambazo sijabariki ndio waonekane kuwa wamefaulu kuliko wengine. Wale walio wanyenyekevu pekee yao ndio wamtafutao Bwana kuwapa majibu kuhusu maisha yao na kukutana na mahitaji yao. Wanaziacha tamaa za kutaka kufuata ulimwengu ili wajionyeshe kwa wenzao.
Wakati unapojikusanyia mali au kujitengenezea jina duniani, hata kupitia kwenye huduma ya Bwana, ni wewe unayetaka kukubaliwa na wengine walio karibu nawe. Hayo siyo mapenzi ya Bwana. Hayawezi kuwa mapenzi ya Bwana. Wanangu wanyenyekevu hunitafuta katika mahitaji yao ya kila siku nami huwakomboa. Hivi ndivyo niwafunzavyo imani. Wakati wanangu wanapambana wakitumia nguvu zao wenyewe ili wafaulu maishani, wanafeli maanake sitawatunukia wale walio nje ya mapenzi yangu. Ingawa wataonekana sawa na kila kitu laini lakini huo ni usalama wa uongo.
Pia, huwa nawaacha wafeli ndipo watambue kuwa wananihitaji. Nahitaji kuwa tamaa ya mioyo yao. Mimi ndiye jibu kwa yote. Vingine vyote ni matumaini ya uongo, yanayowaongoza wanangu nje ya mapenzi yangu.
Ndio, hawa ni wana wenye kiburi wanaopambana kwa njia zao wenyewe bila ushauri wangu, bila kunijua na bila kuniamini. Hii inawafanya wawe na utoshelezaji duni. Endeleeni kupambana. Ndio wanangu, pambaneni na mtatoka mkiwa tupu, mkitamani mengine zaidi bila kutosheka. Mtaendelea kuwa na tamaa, msielewe mnachokitamani. Mimi ndiye “hicho msichokielewa”. Mimi ndiye njia ya pekee ya kutosheka. Kutosheka kiroho, kimwili, na kimoyo.
Natosheleza, nakamilisha na ninamaliza. Najaza mapengo yaliyomo mioyoni mwa binadamu. Hakuna kitu kinachoweza kufanya hivyo, hata binadamu hawezi. Huu ndio msingi wa kiburi na dhambi inayotokana na kiburi. Moyo unaotafuta pahali pote ila kwa Mungu. Tupu, pweke na kutotosheka ndiyo matokeo ya moyo kama huu ulio na kiburi. Maisha ya huzuni ambayo Mimi Mungu sikutaka viumbe vyangu nilivyoviumba viishi.
Kiburi. Dhambi mbovu isiyo na upendo kwa njia yoyote ile. Hakina upendo na yeyote. Unyenyekevu kwa upande mwingine hupenda. Haujipendekezi. Hautawali wengine. Hungoja wengine watumikiwe kwanza. Huenzi wengine kujiliko. Hautumii wengine kwa manufaa yake. Haujigambi na sio fidhuli. Hauna maringo wala majivuno. Unyenyekevu wapendeza, ni mkarimu, ni wenye umbo zuri, wenye upendo, wenye kujali, kama Mungu, kama Kristu na humtafuta Mungu.
Unyenyekevu hautawali wengine wala kujilazimisha kwa cheo. Hungojea wakati wake. Una upendo wakati wote. Hautafuti kuwanyanyasa wengine ili uwe juu. Huwatafutia wema waliomzunguka.
Mbona unyenyekevu ni kitu bora kwangu mimi Mungu? Nafurahia wakati wanangu wananyenyekea mbele zangu. Hiyo inaonyesha heshima na imani kwangu mimi Mungu wao. Wananitumainia mimi ili niwatimizie mahitaji yao yote. Wanaondoa tamaa ya kutaka kujitafutia majibu kwa maisha yao hao wenyewe kupitia nguvu zao, ufanikishaji wao na kujipendekeza kwao. Hawafuati nia zao na kuniacha mimi Mungu wao. Hawajitegemei na kuniacha mimi ambaye ni njia ya kweli. Mimi Mungu wao. Mimi ndimi njia yao ya pekee. Njia ya kweli. Njia.
Wengi wamedanganyika wanaofuata njia zao bila kunisongea na kutafuta mapenzi yangu, ukweli wangu na mwelekeo wangu maishani mwao. Wanafuatilia vile ambavyo dunia inasema vi sawa: pesa, vyeo, kujulikana na kutafuta kujitosheleza kwa njia nyingi zisizofaa. Njia zilizo kando nami Mungu wao. Huo ni udanganyifu wa kiwango cha juu sana.
Sisemi eti msifanye kazi au kuishi maisha. Ninachosema ni kuwa mnitafute kwanza nami nitawaongoza na kuwaelekeza kwa njia zilizo sawa muishipo duniani. Mkifuatilia mipango na ndoto zenu bila mimi kuingilia kati basi mtakuwa mnaenda kando na mapenzi yangu. Hivyo mtakuwa mmejiweka wazi kwa adui wangu na mtakuwa mnaishi kwa dhambi kwa maana hamtakuwa kwenye mapenzi yangu. Hiki ni kiburi na ni uasi. Wengi wanatembea hivi.
Mithali 18:12. Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
Mithali 29:23 Kiburi cha mtu kitamshusha; bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
Mathayo Mtakatifu 23:12. Na ye yote atakaye jikweza atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili atakwezwa.
Waraka wa Yakobo 4:6. Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hivyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Mithali 8:13. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; kiburi na majivuno, ni njia mbovu na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mtu anaketije katika mapenzi yako BWANA? Hivi ndivyo unavyokaa katika mapenzi yangu: Unitii kikamilifu. Kisha nitaziongoza hatua zako kila siku. Uje kwangu kila siku na kuniuliza nikuelekeze, nikuongoze, kama mtoto. Hii ndiyo imani kama ya mtoto. Ulimwengu wawadanganya watu kuwa kujitegemea ndiyo njia ya pekee ya kukuletea ushindi. Huu ni mpango wa adui wangu. Ameudanganya ulimwengu na uongo huu. Wanangu wanafukuza na kukimbiza maisha wakitumia nguvu zao na mipango yao bila kunishauri mimi muumba wao, na kuamini kuwa yote ni salama. Ikiwa inaonekana vyema, basi ni lazima iwe vyema. Lakini huu ni uovu ambao una nia ya kuwaondoa wanangu kutoka kwa njia nyembamba. Mimi pekee ndiye niliye na mwelekeo mwema. Njia iliyo sawa ya wanangu kutembelea nami nawapa mwelekeo huu kila siku.
Yohana Mtakatifu 5:30. Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Ikiwa watu wataendelea kuishi duniani watafanya mipango ya siku za baadaye. Itakuwaje sasa? Ndiyo mwanangu. Wanangu wanaishi duniani, lakini naweza kuwapa mwelekeo kuhusu mipango yao ya siku za baadaye ikiwa watanitafuta. Wakati mwingine jibu huwa: “Tulia na ungoje.” Wale wanangu walio karibu sana nami, watembeao nami kila siku ndio pekee watakaopewa utambuzi. Wanangu walio mbali nami na wananijia tu mara moja moja, sitawabariki. Mimi si Mungu unayemjia mara moja moja kama vile wengine wanaamini. Wengi hunijia wakati wa matatizo kisha wanarudi nyuma na kunisahau. Hawa wana hawanijui.
Mimi ni Mungu anayetamani urafiki wa karibu sana na wanangu. Wanaponikujia mara moja moja ni uovu mkuu. Vuguvu. Ninawatema.
Mathayo Mtakatifu 7:21-23. Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
SURA YA 2: MSIWEKE IMANI YENU KWENU WENYEWE AU KWA WENGINE
Sasa binti, tuanza. Leo nataka kujadiliana nawe kuhusu shida ya ‘ubinafsi’. Kujitosheleza, kujitegemea na kujipendekeza ni dhambi. Inakuzwa na mfumo wa kidunia na adui wangu.
Kujitegemea ni kuiweka nafsi yako mbele badala ya Mungu. Nikutembea kwa mapenzi yako badala ya mapenzi ya Mungu. Ni kama mfungo huu wa siku arobaini ni mapenzi yangu. Watu wanapofanya wapendalo bila kunitafuta kupitia uhusiano wa karibu nami, huwa nje ya mapenzi yangu na hivyo wanaishi kwenye dhambi. Hiyo ni kuniasi. Nataka wanangu wawe katika mapenzi yangu. Wakati mwingine mapenzi yangu hayaonekani yakiwa sawa kulingana na matarajio ya dunia. Dunia inasema fuata pesa, mali, ulinzi na mapenzi ya binadamu. Mapenzi yangu hayalingani na yale dunia huyaona kuwa sawa. Ni tofauti. Lakini mapenzi yangu ni sahihi.
Niliwaumba wanadamu ili waniamini na kutembea kwenye mapenzi yangu. Ili waweze kutembea kwa mapenzi yangu, yafaa wajitolee mhanga mbele yangu na kunitii kwa unyenyekevu na kunitafuta kila siku. Wale wanaonitafuta kwa ukweli kwa kutenga muda wa kuhusiana nami mahali pa siri na kusoma neno langu, watanipata na pia kupata mapenzi yangu. Hii inahitaji uchaguzi. Lazima uchague maanake mambo ya dunia yanaweza kukutoa kwenye njia yangu iliyonyoofu na nyembamba. O! Kuna njia zingine zakuendea lakini zote zitakuteketeza. Njia ya jehanamu ni pana na wengi huifuata. Wachache huipata njia hii iliyo nyembamba na muhimu inayokuja kwangu na kwa uzima wa milele. Wengi hudhani wako kwenye njia nyembamba lakini wamedanganyika. Wanawasikiza wengine waliopotea pia.
Viongozi wangu wengi wamedanganyika na wanawadanganya wengine kwa sababu wanaamini kuwa kufanya kazi nyingi na kukaa kanisani ukijishugulisha ndiko kutakupeleka Mbinguni. Huu ni udanganyifu. Uhusiano wa karibu nami, kunijua na kutumia wakati wako kunijua na kutenga muda kwangu. Huu ndio ufunguo wa usalama wa milele.
Zaburi 91:1. Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Mwili unalishwa kanisani lakini mwili huu hauwezi kufanya kazi vyema bila chakula ninachowapa kwenye mahali pa siri na kwa kutenga wakati wakunijua kwa undani. Hapa ndipo mwili unajengwa kikamilifu. Hapa ndipo nawasilisha mapenzi yangu na maneno yangu kwa kondoo wangu na kuwastahamilisha ndio waweze kupona adui anapowaletea shida.
Ni katika kuwa na uhusiano wa karibu sana nami ndio utakaokuwezesha kustahamili mitego na majaribio ya maisha. Ukijaribu kukabiliana na mambo haya peke yako utapambana na hatimaye ushindwe maanake haujui ninayohitaji ukiwa mbali nami na ilhali mwishowe mimi ndiye hakimu wa wote.
Utaweza je kukabiliana nami wakati wa hukumu ikiwa hujawahi kunikaribia na kujifunza matakwa yangu? Utakaponikabili bila husiano wa karibu nami utakuwa mikono mitupu maanake uliitegemea imani yako, fikira zako, mapenzi yako na utapungukiwa sana. Utakosea.
Warumi 14:12. Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
Usidanganywe. Wengi wa hawa wanaojiita viongozi wangu hawana wakati nami, na hao pia hawatendi
Comments (0)