readenglishbook.com » Religion » Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗

Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗». Author Susan Davis



1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 ... 17
Go to page:
mioyo yao i mbali nami, wanajiamini wenyewe. Huu ni uovu.

Wanaiamini dunia na vitu vya duniani. Hawatembei kwa njia yangu kwa maana hawaniamini. Wangaliniamini, wangalitembea kwenye njia yangu, kwa mapenzi yangu, na kwa njia zangu, kikamilifu. Wanatafuta pande zingine za kwenda. Wanaelekea kwa pande zingine. Wanatafuta majibu kutoka kwa dunia kupitia pesa, umaarufu, usalama, mapenzi na burudani… kila kitu isipokuwa Mimi, Mungu wao! Wajidanganya wasemapo wananiamini, ilhali wanatafuta majibu yao kutoka kwa ulimwengu. Uongo, yote ni uongo. “Mwamini Mungu” wanasema, lakini hawaniachii maisha yao na wanaendelea kukwamilia dunia wakitafuta majibu. Wanaishi kwenye uongo, wajidanganya na hawaoni.

Ndiyo, nawabariki wanangu kwa wingi. Nawanyeshea mvua na kuwaangazia jua kwa wema na waovu pamoja. Lakini wanangu hawaniamini na wanaendelea kufanya usherati na ulimwengu. Huku ni kukirihi. Natamani wana wanaoweka maisha yao chini yangu na kutii na kuniachia maisha yao nakuamini. Wana wanaoiweka mipango yao ya siku zijaazo kwangu na kuyaamini mapenzi yangu kwa ajili ya maisha yao. Wakiwa kwenye mapenzi yangu, hawataabiki wakijishughulisha na kuwa na wasiwasi juu ya kesho. Ninamjali shorewanda, sembuse wanangu wanaoniachia yote na kunitii kikamilifu kwa moyo wote?

Mathayo Mtakatifu 5:44-45. Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombee wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema; huwanyeshea mvua wenye haki na wasio na haki.

Zaburi 4:5. Toeni dhabihu za haki na kumtumaini Bwana.  

Mimi ni Mungu wa kuaminika. Hakuna mwamba mwingine. Mengine yote ni mchanga uzamao. Mimi Mungu adumuye milele. Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Naweza kuaminika. Mbona mnapoteza wakati mkisumbukia mipango yenu wenyewe? Hakuna ajuaye yajayo mbele hata kwenye saa moja ijayo. Mipango yenu yaweza kuharibika kwa kufumba na kufumbua macho. Mbona mnaikwamilia ni kana kwamba inaweza kuwaokoa? Kana kwamba ni ya kutegemewa? Hivyo ni kuabudu miungu wengine kweli!

Mathayo Mtakatifu 7:26. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.

Acheni kuikwamilia hiyo mpango yenu dhaifu. Nipeeni maisha yenu yote. Mimi ndiye nijuaye yajayo. Mimi ndiye nijuaye mtakayofanya kesho.

Matumaini yenu na ndoto zenu nje ya mapenzi yangu yatawaelekeza kwa uteketezi kwa sababu wale walio kwenye mapenzi yangu, wanaonitegemea kwa kila kitu ndio walio salama, salama kweli. Wengine wote wanatembea mbali na mapenzi yangu wakiniasi kwa hivyo hawawezi kwenda mbele na kuwa salama. Hili ni jambo la kusikitisha sana wanangu.

Amkeni na muache kuziamini njia zenu za uasi na muniamini mimi Mungu wenu. Mimi ndiye nijuaye kwenye njia ile nyembamba. Msihadaike mkidhani mwaweza kuipata njia hii bila mimi… huo ni ujinga. Wachache wanaipata njia hii kwa sababu ni wachache sana wanaoacha kuzishikilia njia zao wenyewe. Wale wengine wanadhani njia zao ni mwafaka kwa sababu kila mtu anazifuata, lakini njia ya jehanamu ni pana! Msiwaamini hao wengi wanaowazunguka na hali wamepotea pia. Hamuoni? Ni nini msichokielewa kuhusu haya wanangu?

Mathayo Mtakatifu 7:13-14. Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni pana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi wauingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.

Kwa hivyo, niaminini mimi. Naaminika. Maneno yangu hayakosi kutimia. Kisomeni kitabu changu. Nawakomboa wale ambao wanataka ukombozi. Mimi ni Mungu awakomboao wajitoleao kwangu kikamilifu kwa mioyo iliyovunjika. Kwa hivyo, njooni mkombolewe na mjifunze kuniamini mimi Mungu wenu.

 

SURA YA 5: MSAMAHA

Natuanze tena (Februari 7, 2012). Sasa nataka kuzungumzia kuhusu “Msamaha.” Wanangu, nataka kuzungumzia juu ya jambo hili la msamaha. Wanangu hawana msamaha mioyoni mwao. Wanaweka malalamishi juu ya wengine mioyoni mwao. Siwezi kuwasamehe wasiosamehe. Mnanielewa? Nitawezaje kukusamehe ikiwa hutowasamehe waliokukosea? Je, neno langu halizungumzii haya? Msamaha ni upendo. Kutosamehe kunaleta dhambi zingine nyingi: Uchungu, kulipiza kisasi, hukumu zisizo za kweli na kadhalika. Inampa adui njia ya kuingia ndani na kuwaangamiza. Hii inafanya msiwe na uhusiano wa ndani nami Mungu wenu, na kuwafanya msimpokee Roho wangu. Hili ni kosa kubwa.

Mathayo Mtakatifu 6:14-15. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe nyinyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawa samehe nyinyi makosa yenu.

Ikiwa hauna msamaha kwa wengine, hautakuwa tayari nirudipo. Itatutenganisha. Hautakwenda nami. Achaneni na mambo ya kutosameheana nyuma. Sameheana. Achaneni na hasira mlizo nazo kwa wenzenu. Unafaidika na nini unapomkasirikia mwenzako? Unateseka zaidi kuliko yule uliyemkasirikia. Hauoni haya? Wokovu wenu wa milele una thamani sana kuliko hasira.

Marko Mtakatifu 11:25. Nanyi kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na baba yenu aliye mbinguni awasamehe na nyinyi makosa yenu.

Ichunguzeni mioyo yenu na mjiulize swali hili: Ni lipi la maana sana kukupotezea uzima wako wa milele… kosa ndogo tu? Samehe na uende na uone wingu jeusi likiondoka. Hata kama yule ambaye umemsamehe hatakusamehe, mwombee. Ndiyo, waombeeni maadui zenu. Waombeeni na mioyo mikunjufu na nitaifanya mioyo yenu iwapende wote wanaotaka kuwaumiza. Nitawapa mioyo ya nyama. Itakuwaje mnatarajia watu wasiotembea kwa mapenzi yangu na wasio na Roho Mtakatifu wangu wawe wema kwenu? Lazima muwe watulivu, wakarimu, na wenye huruma kwa watu wasionijua mimi. Ni vigumu sana kwa watu wasionijua, wale wasionijua kwa kweli wawatendee kama wale wanijuao. Hamuoni? Msiwatarajie watu wasio na uhusiano wa ndani nami kuwatendea mema.

Mathayo Mtakatifu 5:44-45. Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa baba yenu aliye mbinguni. Maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Dunia inadhani inaweza kuendelea bila mimi Mungu wake. Inajidanganya. Mimi pekee ndiye ninayeshikilia kila kitu pamoja. Mimi ndiye niletaye njia ya ukweli ya kuishi kwa wanadamu. Dunia hii, inayonitenga, inaishi kwenye mwelekeo wa uongo. Imekuwa na uovu tele.

Hakuna ukweli. Ni maafikiano na ulaghai. Mbali na mienendo yangu minyoofu, binadamu huishi kwenye ulaghai na upotovu. Hakuna yeyote anayeaminika au chochote kinachoaminika. Bi arusi wangu pekee, anayebaki ardhini, na kutembea kwa mapenzi yangu, ndiye aliye kwenye njia nyoofu. Yeye tu ndiye dhabiti na wa kweli. Wengine wote wanatembea kwenye njia isiyoaminika na ya uovu, kwa kila jambo.

Msamaha: Huu ndio ufunguo wa kukufungulia njia ya kurudi kwangu. Msamehe kila mtu. Hakuna kutosamehe ko kote kunaolingana na kupoteza nafasi yako milele.

Luka Mtakatifu 6:37. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni nanyi mtaachiliwa.

Binti yangu, huyu ni Bwana Mungu wako, anayenena nawe. Natuanze, sasa nataka kuwafundisha jinsi ya kuishi na wengine. Wengi wanadharauliana. Hawana utulivu, na heshima. Yote haya yanasababisha ugomvi. Inawafanya wasitosheke na kuleta kuumizana mioyo. Wanangu wana ubinafsi. Wanataka wawe wa kwanza kwa kila jambo. Hawayatilii maanani matakwa ya wengine.

Hawawajali wenzao. Hii inasababisha hasira na mabishano. Wanangu, nina huzunishwa sana na haya. Chanzo cha shida hii ni ubinafsi. Na hii ni kwa sababu ya ukosefu wa unyenyekevu.

Mithali 15:33. Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima. Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Mwenye moyo mnyenyekevu ndiye atakaye weza kuishi na wengine vyema. Lazima mziache tamaa zenu na kuwajali walio karibu nanyi ndio watosheke. Mtahitaji kuchukwa nafasi ya nyuma. Hii ndio njia ya unyenyekevu. Na hii huzaa matunda ya amani, kutosheka na hali nzuri.Wachache sana hujifunza kuishi hivi. Wachache sana huupata ukweli huu. Lakini hii ndiyo njia ya amani, njia yangu. Nawapa sheria hizi za maisha ili ninyi waanangu mwishi kwa amani na kutosheka. Wengi wenu mnakataa kuzifuata kisha mnakuwa na ugomvi na kutotosheka. Mtajifunza lini kuwa njia yangu ndiyo njia njema ya kusafiria? Ninajua kila kitu. Ninajua jinsi wanangu wanaweza kuishi pamoja. Nawapa sheria na kanuni za kuwaongoza kwa nyumba zilizo na amani. Mnahitajika kunifuata na kuziacha njia zenu ili mzifuate sheria zangu.

Zaburi 34:14. Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifuatie.

Tukichagua ubinafsi nyumba zetu zitakosa raha. Niacheni nitawale juu ya nyumba zenu. Niacheni nitawale ndani ya mioyo yenu. Njia yangu ni tulivu, yenye amani, upendo. Nitazifanya nyumba zenu ziwe makao yenye raha kama nilivyowatakia tangu mwanzo. Nipeni mioyo yenu kwa hiari yenu nami nitawanyeshea utulivu. Kaya zenu zitakuwa na uhakika, upendo na amani. Tembeeni kwenye njia za kutosheka, unyenyekevu, na kuwajali wengine ili mzae matunda ya kutosheka. Niacheni nitawale juu ya kaya zenu, na nitawapa maskani yenye raha na furaha.

Zaburi 37:11. Bali wenye upole watairidhi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani.

 

 

SURA YA 6: ISHINI DUNIANI, BALI MSIWE “WA DUNIA”

Natuanze. Leo ninataka kuzungumzia juu ya kuishi duniani. Waanangu wanaishi duniani, bali si lazima wawe “wa dunia”! Dunia ni adui wangu. Nimechukizwa na uovu wake mkuu.

Wanangu, mnaweza kutembea kati ya watu wa dunia bila kushiriki kwenye vitu vya dunia. Dunia itawaongoza kwa njia za upotevu na kuumwa moyo.

Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Mimi ndicho chanzo cha ukamilifu, amani, na utulivu. Msigeukie dunia ili iwape mwelekeo wa maisha yenu. Mtapotoshwa. Ni sharti mnijie mimi niwape mwelekeo. Nishikilieni wakati huu ambao ni muhimu. Nina majibu ya maswali yenu yote.

Ninataka kuwaondolea dhiki na mashaka ila ni lazima mnipe maisha yenu yote. Mkifanya hivyo nitayachukua maisha yenu na kuwakomboa.

Mnaweza kutembea duniani kwa usalama bila ya kuathiriwa na tamaa za duniani, ila mnanihitaji nitembee nanyi. Naweza kuwaongoza mpite kwenye mivuto ya dunia inayoweza kuwa potosha na kuwavuta mbali nami.

Nataka mnitazamie mimi. Myaweke macho yenu kwangu, Mwokozi wenu. Mimi ndiye mlango utakao wapeleka mahali salama. Milango nyingine yote itawepeleka kwa maangamio. Msidanganywe na kuyatoa macho yenu kwangu. Nawapa tumaini kwa dunia hii isiyo na matumaini.

Ooh! Inaonekana kuwa na matumaini, bali kinachoonekana kama kawaida ni udanganyifu.  

Zaburi 25:15. Macho yangu humwelekea BWANA daima. Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

Hizi ni saa za mwisho. Dunia i katika enzi za mwisho. Dunia inakaa kawaida lakini sivyo. Inaelekea kuteketea. Wengi watagundua haya lakini watakuwa wamechelewa. Fungueni macho yenu. Dunia inawapa matumani ya uongo.

Niacheni niwaongoze. Nipeni maisha yenu. Nitayafungua macho yenu kupitia kwa Roho Mtakatifu wangu na mtafanywa upya na kuyaona mambo jinsi yalivyo ndipo mtakapo uona ukweli. Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kuyafungua macho yenu ya kiroho ili muone dunia inavyowadanganya. Ni tayari kuwapa marhamu ya roho ili iwasaidie kubadilika. Mnaweza kuniuliza nami nitawapa. Nipeni mioyo, roho na nafsi na maisha yenu nami niwape macho mnayohitaji ili kutembea salama duniani.

Ufunuo wa Yohana 3:18. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona.

 

SURA YA 7: UNYAKUO NA KARAMU YA ARUSI YA MWANA KONDOO
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 ... 17
Go to page:

Free e-book «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version), Susan Davis [free e books to read online .txt] 📗» - read online now

Comments (0)

There are no comments yet. You can be the first!
Add a comment